Hapa ni kipindi nikiwa nafanya kazi na kikundi cha SEKA
TANZANIA katika kuelemisha jamii kuhusu haki za watoto na shirika lisilo la
kiserikali la Caucus for Childrens Right (CCR) kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka
2013 ambapo tulipata fursa ya kuzunguka katika shule, vijiji na mitaa kila Mkoa
Tanzania tukifikisha ujumbe kwa njia ya sanaa ya maonesho.
Mchezo wa kwanza ulikuwa mwaka 2011 ambao tulizunguka
mikoani tukifikisha ujumbe kwa,
jamii na mchezo huo nilicheza kama mtoto wa
miaka tisa kwa kutumia jina la Elunje, mchezo huu ulimbamba kila mwana jamii
aliye bahatika kuuona maana ulielimisha na kufurahisha japo nilkuwa nateswa na
mama mzazi mama Elunje nakujikuta nimekuwa nunda pasipo mama kujua kama
ananifanya niwe nunda hadi akaamua kunipeleka kwa mama wa kambo akijua
nimeshindikana lakini baada yakuwa kwa mama wa kambo yeye hakunichapa pindi
nimekosea alinielekeza na kunipa adhabu zilizoendana na umri wangu hadi
nikabadilika.
Miongoni mwa scene ambayo sitaisahau na iliyo bamba ni:-
ü ile
niliyo kuwa nikichezea chupi za mama,
ü nyingine
ni ile niliyo uwa kuku kwakujua nimemlaza amesinzia kumbe amekufa,
ü Nyingine
ni ile niliyo kojoa kitandani kila mara,iliyo liza hadhira
ü Nyingine
ni ile niliyo chomwa moto na mama mzazi baada ya kudokoa mboga.
Ukitaka kupata huu mchezo wasiliana nami utaupata ni mchezo
unaochukua dakka 45,nimzuri sanasanasana na mkoa ambao sitausahau ni mkoa wa Tanga
na Dar es salaam,joto lakini Tanga wakati tukiwa kambini tuliibiwa vyombo vyetu
surulia na bakuli.
baadhi ya maonyesho ambayo sitayasahau ni onyesho la Kilakala
Girls, Songea Girls, Nsemembo Tabora, Nkiniziwa Singida, Nzega sehemu ya kupaki
malori yote haya yalifanyika chini ya usimamizi wa MWL.Miranda Rashidi.
Tazama picha ya matukio hapa chini
Mchezo ukiwa umepamba moto na jamii ikiendelea kujifunza |
Moja kati ya sehemu zilizowavutia watazamaji na kukiri kuwa igizo hilo liliwaelimisha |
Hapa nikiwaongoza wenzangu kabla ya kuanza kwa onesho mkoani Morogoo |
Kazi imeanza sasa, twende kazi vijana wangu wakifanya yao jukwaani kabla ya kuanza kwa onesho |
Vijana wa SEKA TANZANIA ndani ya Jezi tukianza kazi ya kuwaita wananchi kuja kujumuika nasi ili wapate elimu |
Wananchi wakifuatilia kwa makini kile tulichokua tunakifanya katika kutoa elimu ya haki ya mtoto |
No comments:
Post a Comment