Moja ya screen shoot ikionesha nilivyotokelezea kwenye moja ya video ya wimbo wangu katika album yangu inayokujia hivi karibuni |
Hii ni moja ya maandalizi ya albam ya mziki wa asili itakayo
kuja hivi karibuni ambayo nimeshirikiana na wana kikundi wenzangu AGESTA,
Albam hii imebeba nyimbo nane,ambazo zimeimbwa kwa makabila tofauti
tofauti za hapa Tanzania.
nyimbo hizi zimebeba jumbe zinazohusu jamii kwa ujumla
nyimbo hizi ni,
;
ü Agesta,
ü Karibu Tanzania,
ü Natasha,
ü MBULA
YA MAWE,
ü Susubha,
ü Bhusunghu,
ü Ung'ang'anile
moto,
ü Mazingira.
kazi hii ni kazi ambayo ina mapito mengi sana tangu nilipo
anza na producer Soja B, kikundi changu cha Agesta na Camera man wetu
imenifanya nijifunze mengi zaidi kupitia methali ya mvumilivu hula mbivu kwakua
haijatoka sitaizungumzia sana kwa sasa siku ikifika ya kuizindua nitawaambia
mapito yake na ni mambo gani niliyokutana nayo yenye kukatisha tamaa na pia
yenye matumaini.
Albam hii japo niya kwanza naamini ni tofauti maana miondoko
yake nilijitahidi nisije nikafanishwa na msanii yeyote duniani, japo mziki na
vifaa ni vilevile naamini producer wangu alijitahidi kila namna kutofautisha na
kunielekeza ili kuonyesha utofauti zaidi.
kwahiyo ndugu zangu kaeni mkao wa kula muda wowote kuanzia
sasa nitawajulisha ni lini tunaizindua naamini ni kazi ambayo mtaipokea maana
hakuna asiye penda mziki wa kiasili japo wasanii wa mziki wa asili sio wengi
kama miondoko miingine hivyo naomba nipokeeni na mtupokee kikundi cha Agesta kwani tuna mitazamo mizuri.
Album hii inakaribia
kuisha kwahiyo wapenzi na mashabiki wa muziki wangu na kazi zangu zote za sanaa
kaeni mkao wa kula kwani nimewaandalia kitu cha tofauti kabisa katika tasnia ya
muziki wa asili.
Hizi ni baadhi ya picha za namna video za nyimbo zangu zitakavyokua :-
No comments:
Post a Comment