Ni msanii wa maigizo na mwimbaji wa nyimbo za Asili na Bongo fleva pia ni mshauri wa masuala ya sanaa.
Nilianza maisha ya sanaa tangu nikiwa na umri wa miaka,
9 kwa kuanza kuimba na kuigiza kanisani na shuleni na baada ya kufika sekondari kipaji kingine cha mpira na kuimba mashairi vikaongezeka.
Mnamo mwaka 2007 ndipo kwa mara ya kwanza niliingia studio na kurekodi nyimbo ya kwanza iliyojulikana kwa jina la innoncensia na baadae nikarekodi nyimbo iliyoenda kwa jina la gharama.
Mnamo mwaka 2009,nikajiunga na kikundi cha sanaa cha Agesta kilichopo Arusha Tanzania na mwaka 2010 nikabahatika kujiunga na kikundi cha SEKA THEATER TANZANIA,tukafanya kazi na shirika lisilo la kiserikali la CCR (Caucus for Childrens Right) tukihamasisha namna ya kuwalinda watoto na tulizunguka Tanzania nzima tukiigiza mchezo ambao niliigiza kama mtoto wa miaka tisa nikiitwa ELUNJE na mchezo ulikuwa na jina hilohilo la ELUNJE pia mchezo mwingine nikiwa manju ulioenda kwa jina la PWAA .
Na baada ya hapo pia tulifanya michezo ndani ya basi ziendazo mikoani kampeni hii( 50% campaign Invisible and Forum Theater) ilinifanya kuijua nchi yangu ya Tanzania.
Tofauti na hiyo naimba mziki wa ASILI ambapo nilijifunza kucheza ngoma za kitamaduni nikiwa kikundi cha AGESTA hadi nikaanza kutunga nyimbo zangu na kufanikiwa kurekodi na Producer wangu SOJA B,albam inayojulikana kwa jina la MBULA YA MAWE,ikimanisha majanga yanayoikumba nchi yetu ya Tanzania na watu wake,
Ndani ya albam hii imebeba nyimbo nane ambazo ni:-
ü Agesta,
ü Karibu Tanzania,
ü Natasha,
ü MBULA
YA MAWE,
ü Susubha,
ü Bhusunghu,
ü Ung'ang'anile
moto,
ü Mazingira.
No comments:
Post a Comment